Dkt.Mwinyi achukua fomu ya Urais Zanzibar

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ambaye pia ni Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), leo Agosti 30,2025 amechukua fomu ya uteuzi wa kuwania kiti cha Urais wa Zanzibar katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Dkt. Mwinyi ameambatana na mke wake,Mama Mariam Mwinyi pamoja na familia na viongozi mbalimbali wa CCM wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Dk.Mohamed Said Dimwa pamoja na wanachama na wakereketwa wa maendeleo waliokusanyika kwa wingi kushuhudia hatua hiyo muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news