DAR-Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na Mgombea Mteule wa CCM kwa nafasi ya Urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 28,2025 katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam ameshiriki katika Uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi 2025.
Kampeni hizo zimezinduliwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, ambaye pia ni Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Mgombea Mwenza, Dkt. Emmanuel John Nchimbi.








