Dkt.Mwinyi kuchukua fomu Agosti 30,2025

ZANZIBAR-Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo Agosti 30,2025.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano Makao Makuu ya CCM Kisiwandui uliopo Mkoa wa Mjini Magharibi, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, Komredi Khamis Mbeto amesema,Dkt.Mwinyi atachukua fomu katika ofisi za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kufuatia taratibu na mwongozo uliowekwa na tume hiyo.

Amesema kuwa,kwa mujibu wa ZEC, wagombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar, Uwakilishi na Udiwani wanatakiwa kuchukua fomu kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 10, 2025, ambapo uteuzi wa wagombea utafanyika Septemba 11, 2025 na kufuatiwa na kuanza rasmi kwa kampeni.

Mbeto ameeleza kuwa,safari ya kuchukua fomu ya Dkt.Mwinyi itaanzia nyumbani kwake Migombani, kisha kuelekea Ofisi za ZEC akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa CCM.

Baada ya kukamilisha taratibu hizo, atarejea Makao Makuu ya chama kupitia gari la wazi, na hatimaye kuelekea katika Kiwanja cha Mau kwa ajili ya kuzungumza na wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news