Dorothy Semu ajiondoa,Luhaga Mpina kuwania Urais Oktoba 29,2025

DAR-Katika kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha ACT Wazalendo kilichofanyika tarehe 5 Agosti 2025 katika Ukumbi wa Hakainde Hichilema, Chama kilipokea taarifa rasmi ya kujitoa kwa Ndugu Dorothy Jonas Semu kutoka kwenye mchakato wa kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo.Dorothy Semu, ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, aliwasilisha hoja zake mbele ya Halmashauri Kuu na kueleza kuwa uamuzi wake umetokana na wajibu wa kiuongozi wa kuhakikisha chama kinabaki imara na kushikamana katika azma ya kuiondoa CCM madarakani kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Alisisitiza kuwa kwa kuzingatia mazingira ya kisiasa ya sasa nchini, hatua yake inalenga kufungua njia kwa uteuzi wa mgombea ambaye ataiunganisha ACT Wazalendo na wananchi kwa ujumla katika mapambano ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini Tanzania.

Halmashauri Kuu ilipokea na kuridhia kwa heshima kubwa hatua ya Ndugu Dorothy Semu, na kumpongeza kwa ujasiri na uadilifu alioonesha katika kipindi chote cha mchakato wa awali wa uteuzi wa wagombea wa urais.

Kutokana na kujitoa kwa Dorothy Semu, Halmashauri Kuu ya Taifa ilipendekeza majina mawili ya wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni Aaron Kalikawe na Luhaga Mpina.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news