ZANZIBAR- Aliyekuwa Mbunge wa Kisesa mkoani Simiyu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Luhaga Joelson Mpina amejiunga rasmi na Chama cha ACT Wazalendo.
Mpina ambaye katika Serikali ya Awamu ya Tano, pia aliwahi kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Awali,ameonekana katika picha na video zilizosambaa mitandaoni, akijiandikisha kupitia mfumo rasmi wa chama hicho uitwao Kiganjani, mbele ya Kiongozi wa ACT Wazalendo Taifa, Dorothy Semu.







