DAR-Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi,Dkt.Samwel Shelukindo imeeleza kwamba, imepokea barua kutoka kwa Katibu Mkuu, Kiongozi Balozi Dk Moses Kusiluka ikitaarifu kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyo nayo chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametengua uteuzi wa Hamphrey Polepole, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba na kumuondolea hadhi ya ubalozi.
.webp)