Maendeleo ya elimu ni mkombozi wa Taifa lolote duniani-Waziri Mkuu

LINDI-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa maendeleo katika sekta ya elimu ndio mkombozi na mafanikio ya Taifa lolote duniani.
Amesema, kwa kutambua hilo, uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan uliamua kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu bora katika ngazi zote.

Amesema hayo wakati alipozungumza na wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia iliyopo Ruangwa mkoani Lindi, wakati wa hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa iliyofanyika mwaka 2025.
“Mliopo shuleni na mnaokuja, tambueni kuwa tuna maeneo muhimu ya kuwaelimisha, mtapata elimu iliyo bora na imara itakayowapa maarifa na ujuzi ili muweze kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii na kiuchumi.”

Amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita imefanya maboresho ya mitaala kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya kiuchumi yaliyopo duniani ikiwemo mahitaji makubwa ya ajira kwa vijana.

“Mabadiliko haya yameifanya mitaala yetu itakayofundishwa shuleni kila mwanafunzi akimaliza ana uwezo wa kutumia mazingira alimo na taaluma aliyonayo kuyabadilisha kuwa uchumi.”
Akisoma matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2025, Makamu Mkuu wa Shule Amon Chalamila hiyo amesema kuwa shule hiyo ilisajili wanafunzi 188 ambapo wote walifanya mitihani na wanafunzi 90 walipata daraja la kwanza, wanafunzi 95 walipata daraja la pili, wanafunzi watatu walipata daraja la tatu na hakuna mwanafunzi aliyepata daraja na nne na sifuri. “Ufaulu huu ni sawa na GPA ya 2.34”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news