Luhaga Mpina kuwania Urais wa Tanzania kupitia ACT Wazalendo

ZANZIBAR-Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza rasmi majina ya wagombea wa nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, kufuatia kikao maalum cha Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika tarehe 5 Agosti 2025 katika ukumbi wa Hakainde Hichilema.
Luhaga Joelson Mpina.

Katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya Chama ilijadili na kupitisha mapendekezo ya wagombea watakaowakilisha ACT Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania majina mawili yamependekezwa kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni Aaron Kalikawe na Luhaga Mpina.
Aaron Kalikawe.

Wagombea hawa wawili watawasilishwa kwa Mkutano Mkuu wa Taifa wa chama kwa ajili ya kupigiwa kura na mmoja wao atachaguliwa kuwa mgombea rasmi wa urais kupitia ACT Wazalendo.





Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news