Magazeti leo Agosti 12,2025

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kongwa kimetangaza kuanza tena mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kongwa, kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge na Mbunge wa jimbo hilo, Job Ndugai kilichotokea Agosti 6,2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Kongwa, Julius Lepupuma zoezi hilo litakuwa la siku moja na litafanyika Agosti 12, 2025 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni, ambapo fomu zitapatikana katika ofisi ya CCM Wilaya ya Kongwa na zitatolewa na Katibu wa Wilaya.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, gharama za fomu zitaendelea kuwa kama zilivyoanishwa kwenye Kanuni za Uongozi katika Vyombo vya Dola toleo la 2025, huku ikisisitiza masharti kwa waombaji ikiwemo kuwa wanachama hai wa CCM wenye akili timamu na waliolipia ada.

Aidha, imekataza wanachama kuandaa misafara ya magari, pikipiki, baiskeli, ngoma au matarumbeta kwa ajili ya kumsindikiza mgombea kuchukua fomu, pamoja na kuwaleta wapambe kwa lengo la kufanya sherehe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news