MTAALAMU wa vita vya kielektroniki wa Kiukreni Serhiy Beskrestnov ametangaza kuwa ubongo na antena iliyotengenezwa na China yenye vipengele 11 vya kuzuia msongamano "Anti-jamming" ambayo ni sehemu ya msingi ya ndege zisizo na rubani za mfululizo wa Shahed, sasa inapatikana kwa kununuliwa kwenye jukwaa kuu la Kichina la e-commerce, Alibaba na AliExpress.
Antena, yenye bei ya karibu $3,290, imeundwa kulinda mifumo ya urambazaji ya ndege isiyo na rubani "Drone Navigation System" dhidi ya kuingiliwa kwa vita vya kielektroniki, kuruhusu Shaheds kugonga malengo kwa usahihi hata ndani ya maeneo inayolindwa na mifumo ya hali ya juu ya kieletroniki.














