Wakulima Mkinga wanufaika na mafunzo ya kilimo bora cha mwani

TANGA-Vikundi 26 Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga vimejengewa uwezo juu ya kilimo bora, utunzaji kumbukumbu, kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao pamoja na masoko ya zao la mwani.
Vikundi hivyo vya wakulima vinahushisha wanawake, vijana na wazee wanaojihusisha na kilimo cha zao la mwani Wilaya ya Mkinga.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa nadharia na vitendo ambapo wanavikundi wameweza kupata ujuzi kwa nadharia kisha mafunzo elekezi kwa vitendo ya namna ya kulima kwa ubora zao hilo.

Mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Serikali ya Japan pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kuratibiwa na Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini,Tawi la Mwanza kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa lengo la kuwafikiwa wakulima wa zao la Mwani ili kuinua vipato vyao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news