TANZANIA imepata heshima nyingine kubwa kimataifa baada ya Bi.Irene Eliakim Maswi kuchaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Wanafunzi Madaktari (IFMSA) kwa kipindi cha 2025/2026.




Bi.Maswi ambaye alianza safari yake ya uongozi katika Chuo Kikuu cha KCMC kwa kushika nafasi ya Rais wa Chama cha Madaktari Wanafunzi Tanzania (TAMSA), ameendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania katika majukwaa ya kimataifa sekta ya afya.
Uteuzi wake umetajwa kuwa alama ya matumaini kwa wanafunzi wa tiba nchini na barani Afrika, ukionyesha wazi kuwa vijana wa Kitanzania wana uwezo wa kushika nafasi muhimu duniani na kuchangia kwa vitendo katika maendeleo ya sekta ya afya.
TAMSA na jumuiya ya wanafunzi wa tiba nchini wamepongeza mafanikio hayo wakisema yanatia moyo kwa kizazi kijacho cha wataalamu wa afya kushiriki katika uongozi na mabadiliko ya kijamii barani Afrika na duniani kote.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo














