MBEYA-Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Mbeya katika Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Katika ziara hiyo, Mhe. Mtaka alipata maelezo kutoka kwa wataalamu wa Benki Kuu kuhusu majukumu yake mbalimbali, hususan utekelezaji wa sera ya fedha na udhibiti wa mfumuko wa bei, pamoja na hatua nyingine zinazolenga kuhakikisha uthabiti wa uchumi wa nchi.
Aidha, ameipongeza Benki Kuu kwa jitihada zake za kuelimisha umma na kuhimiza ushiriki wa wananchi katika maendeleo ya uchumi wa taifa.

