Makumbusho ya BoT ni nyenzo muhimu ya elimu kwa umma-Dkt.Mpango

DAR-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuanzisha Makumbusho ya Benki Kuu ya Tanzania inayolenga kuelezea historia ya fedha nchini na maendeleo mbalimbali ya shughuli za Benki Kuu kwa muktadha wa tulikotoka, tulipo na tunakoelekea.
Akizungumza baada ya kuzindua rasmi makumbusho hiyo Dkt. Mpango ameielezea kuwa ni nyenzo muhimu ya kuelimisha umma hususan vijana ili wapate uelewa wa historia na mageuzi mbalimbali yaliyofanyika katika sekta ya fedha.

“Hongereni kwa kazi kubwa na nzuri mlioifanya. Ninapowapongeza, nawaomba pia muwahamasishe vijana wetu waje kwenye makumbusho haya ili wapate picha halisi ya mageuzi yaliyofanyika nchini katika sekta ya fedha. Hii ni sehemu muhimu sana ya mafunzo,” alisisitiza Dkt.Mpango.

Katika hatua nyingine, Dkt. Mpango, ameipongeza Benki Kuu kwa kuanzisha Maktaba Mtandao akieleza kuwa ni hatua muhimu katika kuhamasisha vijana kupenda kujisomea.

Zinazohusiana

“Kama tunasema asilimia kubwa ya watanzania wapo miaka 35 kurudi chini, maana yake tunahitaji taifa ambalo linasoma. Tuhamasishe vijana wetu kupenda kujisomea.Sasa kwa kuwa kuna huduma kama hizi ina maana mtu haitaji tena kutafuta nakala ngumu anaweza kuingia kwenye simu yake akasoma.”

Dkt. Mpango alifanya uzinduzi wa Makumbusho ya Benki Kuu ya Tanzania na Maktaba Mtandao, tarehe 30 Julai, 2025 katika ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news