Mapya yaibuka mwanafunzi aliyedaiwa kupigwa risasi na Dogo Janja

ARUSHA-Mwanafunzi wa kidato cha nne anayesoma Shule ya Sekondari Sombetini jijini Arusha ambaye hivi karibuni ilidaiwa amepigwa risasi ya mguu na msanii aitwaye Abdulaziz Abubakari (30) mkazi wa Levolosi maarufu Dogo Janja kwa tuhuma za kutaka kumvamia, uongozi wa shule hiyo umesema mwanafunzi huyo aliondolewa shuleni hapo kwa muda tangu Julai 23, 2025, baada ya kukutwa akiwauzia wanafunzi wenzake kashata za bangi.
Bether Jeradi John ambaye ni mkuu wa shule hiyo akizungumza na waandishi wa habari jijini humo amesema, "Mwanafunzi huyu kwasasa yupo nje, kutokana na makosa ambayo aliyafanya Juni 23,2025 yupo nje akisubiri maamuzi ya bodi, kwa sababu alikutwa na kashata za bangi, kithibiti kipo, inazalishwa huko na wananunua huko wanaingia nazo ndani."

Ikumbukwe kuwa katika taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, Agosti 24, 2025, ilieleza kuwa mwanafunzi huyo anayefahamika kwa jina la Bakari Halifa alijeruhiwa kwa kupigwa risasi ya mguu baada ya kutaka kumvamia msaani huyo wakati akiwa anashuka kwenye gari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news