ZANZIBAR-Serikali ya Awamu ya Nane chini ya uongozi thabiti na imara wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi imekuwa ikitumia maarifa na mipango mbalimbali katika kuwaletea maendeleo wananchi kote Unguja na Pemba.
Mwishoni mwa mwaka jana, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alifungua soko jipya na la kisasa la Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B ambalo linaweza kuwanufaisha wafanyabiashara zaidi ya laki moja, ufunguzi huo ulikuwa kati ya miradi mingi ambayo imetekelezwa na Serikali ndani ya miaka mitano ambapo kila sekta imefikiwa hapa Zanzibar, mazuri zaidi yanakuja, tuendelee kumuunga mkono Dkt.Mwinyi.




