DAR-Mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kuzindua msimu mpya wa Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kati ya Young Africans Sports Club na Simba Sports Club itachezwa Septemba 16,2025 jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa TFF, mfumo wa mashindano ya Ngao ya Jamii umebadilika kutokana na marekebisho ya kanuni yaliyopitishwa katika kikao kilichopita cha Kamati ya Utendaji ya TFF.

