Mgombea wa ADA-TADEA achukua fomu za kuwania Urais kwa INEC


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA), Mhe. Georges Gabriel Bussungu. Mgombea huyo aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Ali Makame Issa (kushoto),alichukua fomu hizo leo Agosti 11, 2025 ambapo tume inatarajia kufanya uteuzi Agosti 27, mwaka huu. (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akimkakabidhi mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA), Mhe. Georges Gabriel Bussungu. Mgombea huyo aliambatana na Mgombea Mwenza, Mhe. Ali Makame Issa (kushoto), amechukua fomu hizo leo Agosti 11, 2025 ambapo tume inatarajia kufanya uteuzi Agosti 27, mwaka huu. (Picha na INEC).
Mgombea wa Kiti cha Rais katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA), Mhe. Georges Gabriel Bussungu na Mgombea Mwenza, Mhe. Ali Makame Issa (kushoto) wakionesha mkoba baada ya kukabidhiwa na Tume katika Ofisi za Tume Njedengwa jijini Dodoma leo Agosti 11, 2025 ambapo tume inatarajia kufanya uteuzi Agosti 27, mwaka huu. (Picha na INEC).
Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu. Kulia ni Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar akiwa na Mhe. Magadalena Rwebangira.
Wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa katika ukumbi wa utoaji fomu. Kusho ni Mhe. Jaji Asina Omar akiwa na Mhe. Balozi Ramadhani Omar Mapuri.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele akitoa maelezo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima akitoa maelezo.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima akimpa maelekezo mgombea.
Mgombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Tanzania Democratic Alliance (TADEA), Mhe. Georges Gabriel Bussungu akisaini.
Mgombea Mwenza, Mhe. Ali Makame Issa (kushoto) akisaini kitabu.
Wanachama wa chama hicho wakifuatilia utoaji fomu.
Mgombea akiagana na Mkurugenzi wa Tume.
Mgombea akizungumza na vyombo vya habari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news