Mradi wa Sauti Yetu kuendelea kuibua vipaji vya vijana Zanzibar

ZANZIBAR-Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, ndugu Masoud Juma Haji amesema,Taasisi ya Pamoja Youth Initiative (PYI) inaendelea kuwapatia mafunzo vijana wa Kizanzibari ili kutambua vipaji vyao na kuvielekeza katika maendeleo endelevu ya Taifa.
Akizungumza katika hafla ya utambulisho wa Mradi wa Sauti Yetu uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Migombani, ndugu Masoud amesema, ushirikiano kati ya Wizara na PYI utasaidia kuwafikia vijana wengi zaidi katika mikoa mitatu ya Unguja.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa PYI, Rashid Mwinyi amesema,mradi huo unalenga kuongeza ushiriki wa vijana katika vyombo vya maamuzi na masuala ya siasa, sambamba na kutoa elimu ya uraia, utawala bora na haki za kidemokrasia.

Ameeleza kuwa, kutakuwa na makongamano, mijadala pamoja na mafunzo maalum kwa vijana walioko katika nafasi za uongozi ndani ya vyama vya siasa na asasi za kiraia.

Aidha, amesema mradi huo pia utawajengea uwezo waandishi wa habari kuripoti habari za uchaguzi kwa weledi.

Mradi wa Sauti Yetu unatekelezwa kwa muda wa miezi tisa hadi mwezi Aprili mwaka 2026 na umefadhiliwa na Shirika la Forum Syd kutoka Sweden.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news