DAR-Mwandishi mkongwe wa habari na aliyewahi kuitumikia BBC World Service nchini Tanzania, Erick David Nampesya, amefariki dunia huko Kibamba, Dar es Salaam.Awali, alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mloganzila jijini humo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa jamaa zake wa karibu, marehemu Nampesya alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis), ingawa pia aligundulika kuwa na vidonda vya tumbo.
Nampesya aliyezaliwa mwaka 1969, na aliyekuwa akiripotia Idhaa ya Kiswahili ya BBC, alikumbwa pia na majeraha makubwa kichwani baada ya kuanguka vibaya, anguko ambalo alilielezea mwenyewe takribani miezi miwili kabla ya kifo chake.
.jpeg)