Naibu Katibu Mkuu Omolo aipongeza Wizara ya Fedha na taasisi zake

DODOMA-Naibu Katibu Mkuu anayesimamia masuala ya Huduma za Hazina, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, ametembelea Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni jijini Dodoma ili kujionea huduma zinazotolewa na wizara pamoja na taasisi zake.
Bi. Omolo ameipongeza Wizara na Taasisi kwa kushiriki katika Maonesho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “ChaguaViongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo na Uvuvi2025’’, ili kufikisha elimu kwa wananchi hasa katika sekta ya kilimo ili kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.
‘‘Hongereni sana kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuelimisha wananchi katika maonesho haya, hakika elimu mnayoitoa italeta tija katika utekelezaji wa majukumu ya wananchi ya kila siku, hivyo kuchangia katika ukuaji wa sekta za kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na uchumi kwa ujumla,’’alisema Bi.Omolo.

Wizara ya Fedha pamoja na Taasisi zake imetoa elimu kwa wananchi kuhusu Bajeti ya Serikali, Sera, uwekezaji, pensheni na mirathi, ununuzi wa umma na ugavi, masomo ya vyuo vya elimu ya juu, mifumo ya fedha, takwimu, rufaa za kodi, usuluhishi pamoja na huduma za kibenki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news