Njooni banda la NIRC maonesho ya Nanenane mjifunze mambo mazuri-Mndolwa

DODOMA-Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) inashiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Nananane 2025 katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, ambayo yamenziduliwa Agosti Mosi,2025 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshmiwa Dkt.Philip Isdor Mpango.
Aidha, tume imetoa wito kwa wakulima na wadau wote wa kilimo kushiriki kikamilifu katika kujifunza na kuhamasisha matumizi ya rasililimali ya maji kupitia teknolojia za kisasa za umwagiliaji.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Agosti 2,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Bw.Raymond William Mndolwa.

"Tume inatambua umuhimu wa kuendeleza sekta ya kilimo kupitia umwagiliaji, kama sehemu ya mkakati wa wa kuhakikisha usalama wa chakula, kuongeza kipato cha wananchi na kukuza mchango wa kilimo katika pato la Taifa na maelekezo ya viongozi wa Kitaifa, hususani Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango, aliyeelekeza taasisi za umma kuimarisha elimu,utafiti na teknolojia zinazoleta tija kwa wakulima,Nane Nane 2025 ni fursa mahsusi ya kuwafikia wananchi kwa elimu ya vitendo na teknolojia bunifu."

Mndolwa kupitia taarifa hiyo amefafanua kuwa,tume imejipanga kutoa mafunzo, maelezo ya kitaalamu,na kuhamasisha matumizi ya umwagiliaji ili wakulima waweze kuongeza uzalishaji,kipato na ustawi wa familia zao na taifa kwa ujumla.

Aidha,tume inashirikiana na sekta binafsi kusambaza teknolojia mpya za umwagiliaji, zitakazo tumia maji kwa ufanisi na kuleta tija kwenye kilimo, kufuatilia utekelezaji wa sera za kilimo biashara,na kuendeleza matumizi bora ya maji na mbinu za kukabili mabadiliko ya tabianchi, kwa lengo la kuifanya Tanzania iwe kitovu cha uzalishaji wa chakula barani Afrika na duniani kote.

"Wananchi, wakulima, na wadau wa sekta ya kilimo wanakaribishwa kutembelea banda la Tume katika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma, kujifunza zaidi kutoka kwa wataalamu wa Tume, kushuhudia ubunifu wa kiteknolojia, na kuungana katika mwelekeo mpya wa kilimo cha kisasa na endelevu, kupitia kilimo cha Umwagiliaji,"amefafanua Bw.Raymond William Mndolwa kupitia taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news