TARURA na jambo muhimu kwa jamii ndani ya Nanenane 2025

DODOMA-Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inashiriki Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Nzuguni jijini Dodoma.
TARURA inashiriki maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kuhusu kazi na majukumu yake pamoja na kupokea maoni na malalamiko kutoka kwa wananchi.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TARURA, Bi.Catherine Sungura amesema kuwa, TARURA imejipanga kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wanayoyasimamia yanayohusu ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini.
Kwa mujibu wa Sungura baadhi ya maeneo hayo ni pamoja usimamizi wa matengenezo ya kawaida, matengenezo ya maeneo korofi shughuli za maabara,mazingira na jamii.

"Kupitia wataalamu wetu ambao wapo katika banda letu tumejipanga pia kutoa elimu kwa wananchi na wadau wetu wengine namna wanavyoweza kushirikiana na TARURA kuwezesha matengenezo madogo madogo ya barabara kupitia vikundi vya kijamii," amefafanua Sungura.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kutembelea Banda la TARURA na mabanda mengine ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI ambayo yanapatikana katika hema linalosomeka "Government Zone Pavilion 2" ili wapate elimu na ufahamu kuhusu taasisi hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news