Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaendelea kuwahudumia wananchi Maonesho ya Nanenane viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma


Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Hosana Mgeni akiwapitisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mtakatifu Gabriel kwenye kitabu chenye mkusanyiko wa sheria walipotembelea banda la Ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane Kitaifa yanayofanyika Viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma.
Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakisaini kitabu cha wageni wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma.
Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, wakitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma.
Mawakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakitoa elimu ya msaada wa kisheria kwa baadhi ya wananchi waliotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma.
Wakili wa Serikali wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Doreen Mhina akitoa maelezo kuhusu masomo ya kuzingatia ili kuwa Wakili wa Serikali kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlangwa walipotembelea banda la Ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma.
Mwandishi wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ndugu Abtwalib Makame akiangalia kipeperushi kinachoelezea majukumu ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali alipotembelea banda la ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news