Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemtembelea na kumjulia hali Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Ndg. Abdallah Juma Abdallah Sadala (Mabodi), aliyelazwa katika Hospitali ya Benjamin William Mkapa, Dodoma tarehe 22 Agosti 2025.

