Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo leo Agosti 11,2025 Ikulu,Zanzibar katika kikao maalum na mawaziri mbalimbali akiwemo Mhe.Rahma Kassim Ali, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Mhe. Shariff Ali Shariff, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji,Mhe.Tabia Maulid Mwita, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, pamoja na Taasisi ya Ofisi ya Rais, Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (ZPDB), kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja kuhusu matumizi sahihi ya ardhi katika maeneo ya uwekezaji Fumba.


