Rais Dkt.Mwinyi atunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) katika Uchumi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) katika Uchumi iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU), ambayo ilitangazwa rasmi Desemba 2024 katika mahafali ya Chuo hicho.
Mkuu wa Chuo hicho, Mhandisi Abdulqadir Othman Hafez, alikabidhi rasmi Shahada hiyo kwa Rais Dkt. Mwinyi Ikulu Zanzibar leo tarehe 25 Agosti, 2025.
Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amepewa heshima hii kwa kutambua mchango wake katika kuimarisha miundombinu, matumizi sahihi ya rasilimali zilizopo nchini kwa ustawi wa wananchi, uchumi wa buluu, uwezeshaji wananchi, sera wezeshi za kijamii kama pensheni jamii, fursa za ajira huku uchumi wa Zanzibar ukiendelea kukua kwa kasi zaidi
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amekipongeza Chuo hicho kwa kuthamini na kutambua juhudi zake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Zanzibar, hatua ambayo ameieleza kuwa itamwongezea ari ya kuendeleza maendeleo zaidi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news