ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi leo Agosti 29,2025 amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA).
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said ambapo hatua hiyo imechukuliwa kuanzia leo.

