DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

Viongozi Wateule wakiapa Kiapo cha Maadili kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye hafla ya Uapisho wa Viongozi mbalimbali, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2025.Rais Dkt. Samia amesema hayo wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali wa Serikali aliowateua hivi karibuni katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha CPA. Amos Gabriel Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2025.Aidha, Rais Dkt. Samia amewataka viongozi kushirikiana na watendaji wengine wa Serikali kufanya kazi kwa ukaribu na wananchi ili kuzitambua na kuzishughulikia kero zao kwa wakati.
Viongozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2025.Halikadhalika, Rais Dkt. Samia ametoa rai kwa Wakuu wa Mikoa kuhamasisha ushiriki wawananchi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 katika mazingira ya amani na utulivu.
Akizungumzia jitihada za Serikali za kuboresha utoaji wa huduma na kuendeleza miundombinu katika Mkoa wa Dodoma, Rais Dkt. Samia amesema Serikali imeweka mazingira mazuri yanayovutia wawekezaji na kuwataka viongozi wa Mkoa huo kuendeleza jitihada hizo zinazoimarisha ustawi wa wakazi wa Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Khatibu Malimi Kazungu kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2025.Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amewataka Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma kusimamia weledi, uwajibikaji na uadilifu katika utumishi wa umma ili kufikia matarajio makubwa ya Watanzania yaliyowekwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Deo Osmund Mwapinga kuwa Balozi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Laurean Josephat Ndumbaro kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma tarehe 26 Agosti, 2025.Viongozi walioapishwa ni CPA Amos Gabriel Makalla aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dkt. Khatibu Malimi Kazungu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma; Dkt. Deo Osmund Mwapinga kuwa Balozi; pamoja na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma ambao ni Bi. Salama Aboud Twalib, Dkt. Laurean Josephat Ndumbaro na Bw.Hassan Omari Kitenge.















