Vyama 18 vyakutana na INEC kupanga ratiba za kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

DODOMA-Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imekutana na Vyama vya Siasa 18 vyenye usajili kamili na ambavyo vimesimamisha wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kujadili na kupanga kwa pamoja ratiba ya kampeni za wagombea wa nafasi ya Kiti cha Rais na Makamu wa Rais wa vyama hivyo. Hatua hiyo imekuja baada ya vyama vyote kuwasilisha Tume ratiba zao za kampeni.
Kikao hicho kiliongozwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndg. Ramadhani Kailima na kufanyika katika ofisi za tume Dodoma siku ya Agosti 25, 2025.
Vyama vilivyo shiriki katika kikao hicho ni pamoja na Civic United Front (CUF), National Convention for Construction and Reform (NCCR), Union for Multiparty Democracy (UMD), Chama cha Mapinduzi (CCM), National League for Democracy (NLD), United Peoples’ Democratic Party (UPDP) na National Reconstruction Alliance (NRA), African Democratic Alliance Party (ADA-TADEA).
Vyama vingine ni Tanzania Labour Party (TLP), United Democratic Party (UDP), Madini Kilimo Nishati (MAKINI), Democratic Party (DP), Sauti ya Umma (SAU), Alliance for African Farmers Party (AAFP), Chama cha Kijamii (CCK), Alliance for Democratic Change (ADC) na Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) na Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo).
Kampeni za Uchaguzi zinataraji kuanza Agosti 28, 2025 hadi Oktoba 28, 2025 nchini kote ambapo wagombea watakaoteuliwa na Tume watafanya kampeni za kunadi sera za vyama vyao kutafuta ridhaa ya wananchi kuwapigia kura Oktoba 29, 2025 katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news