ARUSHA-Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga ametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Arusha katika Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayofanyika katika Viwanja vya Nanenane, Njiro.
Katika ziara hiyo,Mhe.Sendiga ameipongeza Benki Kuu kwa jitihada inazofanya katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya kifedha.
Aidha, amesisitiza kuwa, elimu hiyo ni muhimu kwa wananchi kwani inawawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi wa taifa.

