DAR-Shomari Kapombe dakika ya 89 amewapa furaha Watanzania baada ya kuiandikia Taifa Stars bao pekee dhidi ya Mauritania katika michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) 2024.
Ni kupitia mtanange uliopigwa leo Agosti 6,2025 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Ushindi wa leo unaongeza nguvu kwa ule wa Agosti 2,2025 ambapo Taifa Stars iliichapa Burkina Faso mabao 2-0 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa dimbani hapo.
Kwa matokeo hayo, Taifa Stars inaongoza Kundi B kwa alama 6, ikafuatiwa na Burkina Faso wenye alama tatu, Madagascar alama moja,Mauritania alama moja na Jamhuri ya Afrika ya Kati ikiwa haina kitu.

