DAR-Klabu za soka za Tanzania,Simba na Yanga zimepelekwa Botswana na Angola baada ya leo Agosti 9,2025 jijini Dar es Saam, kufanyika droo ya michuano ya CAF ngazi ya klabu (CAF CL na CAF CC).
Simba SC itacheza na Gaborone United ya Botswana huku Yanga ikipangwa kucheza dhidi ya Wiliete Benguela ya Angola.Klabu zote mbili zitaanzia ugenini na kumalizia nyumbani.
Aidha, hii ni droo ya hatua za awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) na Kombe la Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC).
