DODOMA-Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Kongwa, Job Yustino Ndugai amefariki dunia leo Agosti 06,2025 akiwa anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini baada ya kuugua ghafla.
Ndugai amekuwa Spika wa Bunge tangu Novemba 17, 2015 hadi Januari 06, 2022 alipojiuzulu na kuendelea kuwa Mbunge wa Kongwa, nafasi ambayo ameendelea kuitetea kwa kuchukua fomu tena mwaka huu ambapo ameshinda kwenye kura za maoni.
Ndugai ambaye amezaliwa Januari 22,1960 alishinda kura za maoni za Ubunge wa Jimbo la Kongwa kwa kupata kura 5,690 kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025.

