DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole katika kurasa zake mbalimbali za mitandao ya kijamii kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai aliyefariki leo Agosti 06,2025.
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninatoa pole kwa familia, wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi, watumishi wa Bunge na Wabunge wote aliotumikia nao akiwa Spika wa Bunge letu, wananchi wa Kongwa, ndugu jamaa na marafiki."Tuungane pamoja kumuombea kwa Mwenyezi Mungu na kuwaombea familia, ndugu, jamaa na marafiki uvumilivu, faraja na moyo wa ibada katika kipindi hiki kigumu,"ameandika Rais Dkt.Samia.