TARURA Musoma wapongezwa ujenzi wa miradi kulingana na thamani ya fedha

MARA-Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi amewapongeza wafanyakazi wa TARURA wilaya ya Musoma kwa kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanajenga miradi ya miundombinu ya barabara kulingana na thamani halisi ya fedha.
Ndugu Ussi ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa barabara ya Nyabisarye Mahakama kuu Kanda ya Musoma yenye urefu wa mita 700 kwa kiwango cha lami.

Ussi amesema kuwa  Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa lengo la kuwarahisishia wananchi huduma katika maeneno yao ili waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi na kujiingizia kipato.
Kwa upande wake Kaimu Meneja Wilaya ya Musoma Mhandisi Mohamed Etanga amesema jumla ya shilingi Milioni 600.97 zimetengwa kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Nyabisarye- Mahakama Kuu yenye urefu wa Mita 700 kwa kiwango cha lami.

Amebainisha kuwa ujenzi wa barabara hiyo ulianza Oktoba mwaka jana na unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba, 2025.
Mhandisi Etanga ameongeza kusema kuwa barabara hiyo endapo itakamilika itakuwa kiunganishi cha Kata ya Bweri na Kata ya Rwamlimi na kuwa kiungo kikubwa kwa wananchi katika kupata mahitaji ya kijamii kwa wepesi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news