ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa,Zanzibar inahitaji fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo Uchumi wa Buluu, sekta ya miundombinu, afya pamoja na fursa za kibiashara kwa ajili ya kuongeza thamani ya bidhaa za karafuu na mazao ya baharini.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk, aliyefika Ikulu Zanzibar leo Agosti 19,2025 kumuaga baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.





