TEC laidhinisha uteuzi wa viongozi Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (RUCU)

DAR-Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Mmiliki wa Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (RUCU), kupitia Mkutano wake limeidhinisha rasmi uteuzi wa Viongozi wakuu wa chuo ikiwa lengo ni kuendeleza mshikamano, uwajibikaji na ubunifu katika kufanikisha dira na malengo ya Chuo.
Kupitia taarifa rasmi ambayo imetolewa kwa Waandishi wa habari Katika uteuzi huo Sr. Profesa Chrispina S. Lekule ameteuliwa kuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha RUCU, ambapo majukumu yake anatarajia kuanza rasmi Septemba 1, 2025.
Prof. Lekule amepokea uteuzi huo kwa unyenyekevu, na anatarajia kushirikiana kwa karibu na watumishi wa RUCU pamoja na wadau wa elimu nchini katika kuboresha elimu inayojibu changamoto za jamii.
Sambamba na uteuzi wa Makamu Mkuu wa Chuo, TEC pia imethibitisha na kumteua Prof. Alex J. Ochumbo kuwa Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Fedha na Utawala (DVC–FA) vilevile Dr. Pius Peter Mgeni Mweka Hazina wa Chuo ameteuliwa rasmi kushika nafasi hiyo.

Sr. Prof. Lekule ni msomi mwenye sifa na tajiriba ya kimataifa katika elimu ya juu, aliyejikita katika uongozi unaozingatia maadili, ubora wa kitaaluma, na mabadiliko chanya ya kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news