TMA yafikisha elimu kwa wananchi wengi Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki

MOROGORO-Katika Maonesho ya Nanenane Kanda ya Mashariki jamii imepata elimu kuhusu mchango wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa wakulima wadogo.Vilevile namna ya kutumia taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa kupanga shughuli za kilimo ili kuongeza tija na kupunguza hasara.

‎Elimu hiyo ilitolewa kupitia matangazo Mubashara MVIWATA FM, yakirushwa kutoka Banda la Mamlaka ya Hali ya Hewa katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika Uwanja wa Mwalimu Nyerere mkoani Morogoro, hatua iliyosaidia kuwafikia wakulima wengi zaidi hata nje ya uwanja wa maonesho.
Akizungumzia umuhimu wa TMA katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa wakulima wadogo, Meneja wa Mamlaka ya Hali ya hewa Kanda ya Mashariki Bi. Hidaya Senga amesema, kupitia vyombo vya habari na programu mbalimbali wakulima wamekuwa wakipata taarifa kwa wakati.
Pia,Bi.Hidaya Senga, ameishukuru Serikali kwa kuwapatia vifaa vya kisasa vinavyowezesha ukusanyaji na uchambuzi wa taarifa za hali ya hewa kwa haraka na usahihi, jambo linaloboresha utoaji wa tahadhari na taarifa muhimu kwa wakulima na wananchi kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news