TMA yang'ara Maonesho ya Nanenane 2025

MOROGORO- Agosti 8,2025 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imenyakua kombe kupitia Maonesho ya Nane Nane 2025 yaliyofanyika katika Mkoa wa Morogoro. Ushindani wa TMA kupitia kundi la ushindani lililohusisha taasisi za Serikali upande wa Mawakala na Mamlaka za Serikali nchini, umeifanya TMA kuibuka kidedea kwa kushika nafasi ya pili ambapo Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ilishika nafasi ya kwanza na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ikishika nafasi ya tatu.
Aidha, TMA imelipokea kombe hilo kwa furaha kubwa na kutoa shukrani zao za dhati kwa waratibu wa maonesho hayo kwa kutambua mchango mkubwa wa TMA katika kuhudumia wadau mbalimbali kwenye maonesho hayo, ambapo wageni zaidi ya 2942 wameweza kuhudumiwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ya sayansi ya hali ya hewa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news