Ubunge ni kazi ya watu-Dkt.Biteko

GEITA-Dkt.Doto Mashaka Biteko leo Agosti 3, 2025 amefika kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa wilaya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa nafasi ya ubunge wa Jimbo la Bukombe.

Hatua hiyo ni sehemu ya utambulisho wa wagombea wa udiwani na ubunge katika kata za Katente, Ng’anzo, Bulangwa, Namonge, Busonzo, Runzewe Magharibi na Butinzya zilizopo Jimbo la Bukombe.
Akizungumza mbele ya Wajumbe, Mbunge anayemaliza muda wake Dkt. Doto Biteko amesema kuwa amerudi kwao akiamini kwamba wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Wananchi wa Bukombe ndio wanatoa ridhaa kwa mgombea kupata wadhifa huo.
"Nawaambieni ukitaka kufanya kazi ya ubunge rudi kwa watu, maana hii kazi ya ni ya Watu nenda kawaone wenye kazi yao, ndio maana kila nikienda baada ya muda lazima nirudi, nilikuwa narudi kwa watu na mlivyokuwa wema kila ninaporudi mnanipokea vizuri nafarijika.”

Aidha, Dkt.Doto Mashaka Biteko amesema kuwa, miaka mitano iliyopita ilikuwa miaka ya kazi iliyopambwa na ushirikiano wa kutosha miongoni mwa viongozi na wanaCCM jambo lililokiwezesha Chama Cha Mapinduzi kupata heshima kubwa na leo nimekuja kwenu kuwashukuru sana na kwa unyenyekevu mkubwa ninawaomba kura zenu za ndiyo.
“Mimi sitaweka mawakala katika vituo vya kupigia kura kwa sababu sina mashaka na nyinyi watu wema wa Bukombe, bali mawakala wangu mtakuwa ninyi wananchi wenyewe wa Bukombe."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news