.jpeg)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameendelea kuwa kiongozi mnyenyekevu na msikivu, hali inayoendelea kufanya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nane Zanzibar kuendelea kuacha alama kila sekta.
Dkt.Mwinyi amefanikisha mageuzi ya msingi katika sekta mbalimbali Zanzibar, ambayo yameleta majawabu ya changamoto na kero ambazo zilikuwa zinawakabili wananchi huko nyuma, mafanikio haya yanatokana na kujiwekea utaratibu mahususi wa kusikiliza matatizo ya wananchi moja kwa moja kisha kuyapatia ufumbuzi.