DODOMA-Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika mkoani Dodoma leo Agosti 23,2025.
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.







