Menejimenti kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) maarufu kama UTATU wamekutana jijini Dodoma kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji kazi ya mwaka uliopita na kuweka maazimio kwa mwaka huu.