"Leo tunasherehekea Siku ya Vijana Duniani, siku maalum ya kutambua nguvu,ubunifu, na mchango mkubwa wa Vijana katika kuijenga jamii na taifa letu.Vijana ndio nguvu kazi ya leo na viongozi wa kesho.Ndani yenu kuna ndoto kubwa na mawazo mapya kwa mustakabali wa Taifa letu.
"Ninawahimiza muendelee kusimama kidete katika kusaka elimu,maarifa ,ujuzi, na kuwa wabunifu, wachapakazi,na wajasiri mbele ya changamoto. Ndiyo nyinyi mnaoleta mabadiliko katika familia zenu,jamii zenu , na taifa kwa ujumla."Kwa pamoja, tukiwa na mshikamano, nidhamu, na maadili mema ,tukidumisha amani kwa maendeleo zaidi,"ameeleza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar na, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.