Dkt.Biteko aagiza barabara ya mita 900 kujengwa Ngara

KAGERA-Askofu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dayosisi ya Kagera, Darlington Misango Bendankeh ameiomba Serikali kufanikisha ujenzi wa Barabara inayounganisha taasisi mbalimbali za utoaji wa huduma yenye urefu wa mita 900, gari la wagonjwa pamoja na mchango wa ujenzi kanisa ambalo ujenzi wake unaendelea kwa gharama ya shilingi bilioni 1.18.
Kufuatia maombi hayo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amemwelekeza Mkuu wa Mkoa, Mkuu Wilaya na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kufanikisha ujenzi wa kipande hicho huku akitoa ahadi ya gari la wagonjwa katika Hospitali ya Murgwanza baada ya kuwasiliana na Waziri wa Afya, Mhe.Jenista Mhagama.

Dkt. Biteko amesema hayo Agosti 12, 2025 wakati akimwakilisha Mheshimiwa Rais katika Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 40 ya Kuzaliwa kwa Dayosisi ya Kagera iliyofanyika katika Viwanja vya Kanisa Kuu Yohana Mbatizaji - Murgwanza, Ngara Mkoani Kagera.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news