ZANZIBAR-Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wameendelea kutembelea Banda la Benki Kuu ya Tanzania kwenye Maonesho ya Nane Nane Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Dole-Kizimbani, visiwani Unguja, Zanzibar.
Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Shaibu Hassan Kaduara, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar, Bw. Sultan Said Suleiman na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar, Kanali Burhan Zubeir Nassor.
Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Mhe. Shaibu Hassan Kaduara, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Zanzibar, Bw. Sultan Said Suleiman na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar, Kanali Burhan Zubeir Nassor.Katika maonesho hayo Benki Kuu inaelimisha umma kuhusu majukumu yake katika kusimamia ukuaji endelevu wa uchumi na ustawi wa sekta ya fedha nchini.









