DODOMA-Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Dodoma, Dkt.Wilfred Mbowe, ametembelea banda la Benki Kuu katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa jijini Dodoma, na kujionea namna wataalamu wa Benki hiyo wanavyotekeleza shughuli za utoaji wa elimu kwa wananchi.
Katika maonesho hayo, Benki Kuu ya Tanzania inatoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake mbalimbali, kwa lengo la kuwaongezea wananchi uelewa juu ya kazi na wajibu wa Benki Kuu katika kusimamia na kuimarisha uchumi wa taifa.Dkt. Mbowe aliambatana na Meneja wa Idara ya Uendeshaji, Tawi la BoT Dodoma, Bw. Nolasco Maluli, pamoja na Meneja wa Idara ya Fedha na Utawala, Bw. Francis Assenga.
Maonesho ya Nanenane kwa mwaka 2025 yanaongozwa na kaulimbiu: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025”, na yanafanyika katika Viwanja vya Nanenane, Nzuguni – jijini Dodoma, kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025.