DAR-Wadau mbalimbali wa Elimu wamekusanyika leo Agosti 25, 2025 jijini Dar es Salaam katika Kongamano la Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kusherekea mafanikio ya taasisi hiyo tangu kuanzishwa kwake.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima ilianzishwa mwaka 1960 kama kitengo cha masomo ya nje ya darasa cha Chuo cha Makerere, chini ya Chuo Kikuu cha London. Mnamo mwaka 1963, Taasisi hiyo iliboreshwa kuwa idara na kuwekwa chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kongamano hilo linahususha maonesho ya bidhaa za wanakisomo wa Taasisi hiyo zilizotokana na mafunzo ya vitendo na ubunifu wa washiriki.
Aidha, wanafunzi wa Taasisi wameandaa vifaa vya kujifunzia vinavyoakisi mbinu bunifu na shirikishi za elimu ya watu wazima.
Taasisi mbalimbali zinazotoa mafunzo endelevu nchini ikiwemo vyuo vya ufundi, mashirika ya kijamii na wadau wa maendeleo, zinashiriki kongamano hili kuonesha mshikamano na dhamira ya pamoja ya kuendeleza elimu jumuishi na inayolenga matokeo chanya kwa jamii.Kauli mbiu ya kongamano hili ni 𝗘𝗹𝗶𝗺𝘂 𝗯𝗶𝗹𝗮 𝗨𝗸𝗼𝗺𝗼 𝗸𝘄𝗮 𝗠𝗮𝗲𝗻𝗱𝗲𝗹𝗲𝗼 𝗘𝗻𝗱𝗲𝗹𝗲𝘃𝘂.












