Wakulima na wavuvi Zanzibar watakiwa kutumia taarifa za hali ya hewa ili kuleta tija na kuongeza kipato

ZANZIBAR-Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa wito kwa wakulima na wavuvi kutumia taarifa za hali ya hewa ili kuleta tija na kuongeza kipato.
Wito huo umetolewa kwenye Maonesho Nanenane 2025 yanayofanyika katika Viwanja vya Dole Kizimbani,Zanzibar.
Mkurugenzi wa TMA Ofisi ya Zanzibar, ndugu Masoud Makame Faki akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Banda la TMA aliwahimiza wakulima na wavuvi kufuatilia utabiri wa kila siku, utabiri wa msimu pamoja na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinazotolewa na Mamlaka,kwani mkulima hawezi kupata utajiri au ongezeko la pato bila kutumia taarifa za hali ya hewa.Kaulimbiu ni “Kilimo ni utajiri, Tunza Amani, Lima kwa ubunifu”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news